Isimujamii (pia isimu jamii) ni tawi la isimu ambalo huchunguza uhusiano kati ya lugha na jamii.
Aidha inajihusisha na athira yeyote ya jamii kama vile desturi za watu, matazamio, na muktadha, katika nyanja za lugha namna inavyotumika. Neno hili kwa Kiingereza huitwa: Sociolinguistics.
Chini ya taaluma hiyo, kuna matawi mengi yanayoshughulikia uchanganuzi wa vipengele fulani vya uhusiano kati ya lugha na jamii, k.m.
# uhusiano kati ya lugha na utamaduni
# matumizi ya aina tofauti za lugha na mazingira yake, kama lahaja, rejista na mtindo
# matumizi ya lugha tofauti wakati mmoja, kama katika wingilugha, ubadilishaji msimbo na diglosia
# vipengele mbalimbali vya mawasiliano kupitia maoni ya msemaji (tawi hilo pia huitwa isimu amali)
# matumizi ya lugha baina ya jamii za watu tofauti, kama lugha mawasiliano, pijini na krioli
# uhusiano kati ya lugha na siasa katika upangaji lugha na sera za lugha
*TUKI 1990, "Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha", Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
*Massamba, David 2004, "Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha", Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
*Buliba, Aswani, Kimani Njogu & Alice Mwihaki 2006, "Isimujamii kwa Wanafunzi wa Kiswahili", Nairobi: The Jomo Kenyatta Foundation
macha kutokka sauti ana kubali maelezo haya kwani ni vitu viwili vinavyoambatana
*Applied Linguistics Resources on Dmoz
Jamii:Lugha
Mapyourinfo translations allows you to search a foreign language with your own language (translate search) and receive the content also in your language
